Friday 8 June 2018

UKWELI KUHUSU MIGUNO YA WANAWAKE WAKATI WA KUJAMIIANA


 Fahamu ukweli kuhusu milio wanayotoa wanawake wakati wa kujamiana.



Kama wewe ni mwanaume, basi bila shaka

unafahamu ile milio na miguno ya wanawake
wakati wa kujamiiana, na kama wewe ni
mwanamke pia unafahamu kwamba huwa unatoa
milio na miguno hiyo. Ni nini basi kinachopelekea

milio na miguno hii kutolewa? Je milio na miguno
hii ni ya kweli au ni zuga tu, ili kumfanya
mwanaume ajisikie “kijogoo“?
Baadhi ya wataalamu wa masuala ya kujamiiana
na mapenzi walijiuliza pia maswali hayo. Mwaka
jana, Gayle Brewer wa Chuo Kikuu cha Central
Lancashire na Colin Hendrie, wa Chuo Kikuu cha
Leeds waliibuka na utafiti wao waliouita
“Copulatory Vocalization“ (kwa tafsiri
nyepesi-“Milio/sauti za kujamiiana”). Katika utafiti
huo, waliuliza wanawake 71 ambao wanashiriki
tendo hilo mara kwa mara (sexually active) kati
ya umri wa miaka 18 na 48 kwa ajili ya kupata
undani zaidi wa suala hili la kutoa milio wakati
wa kujamiiana.
Wataalamu hao waliweza kubaini kwamba wengi
wa wanawake hao walikuwa wanatoa milio, lakini
sio tu wakati wanafika kileleni (orgasm), bali 66%
walisema walitoa milio, ili kuharakisha wanaume
zao kufika kileleni, na 87% walisema kwamba
walitoa milio, ili kumfanya wanaume ajisikie
“Kijogoo” (boost his self-esteem).
Wataalamu hao waliongeza kusema kwamba
“Wakati mwanamke kwa kawaida hufika kileleni
wakati wa kutomasana, mara nyingi milio ya
kujamiiana imeripotiwa kutokea mara kwa mara
kabla au sambamba na wakati ambao mwanaume
anafika kileleni“. Walisema pia katika utafiti wao
imebainika kwamba wakati mwingine wanawake
walitoa milio na miguno, ili kukabiliana na
kuboheka, uchovu, na maumivu wakati wa tendo
la ndo, kwahiyo basi wanaume inabidi kuwa
makini kwani wakati mwengine kumbe mtoto wa
watu ana umia! Au pengine yupo kwenye zile
harakati za kukuzuga, ili ujione “Kijogoo”?
Wataalamu wanaendelea kusema kwamba tatizo
kubwa ni kwamba jamii imefanywa kuamini
kwamba milio wakati wa tendo la kujamiiana
huusishwa na mwanamke kufika kileleni au
kufurahia tendo hilo, kiasi kwamba imefikia
wanawake kuona ni busara kudanganya (fake)
kwamba wamefika kileleni (wakijua fika kwamba
mwanaume tayari ana amini hivyo) wakati kumbe
hawajafika popote.
Wataalamu wanaonya kwamba sio busara kwa
wanawake kudanganya kwamba wamefika
kileleni, kwani kufanya hivyo kunapelekea
wanaume kufikiri kwamba wanafanya kila kitu
sawa wakati wa mapigo, wakati kumbe sio.
Mwalimu wa elimu ya kujamiiana, Patty Brisben,
anashauri kwamba wanawake watumie miguno/
milio kama “njia ya kuonyesha kwamba
wanafurahia tendo, lakini sio njia ya kuficha
kama tendo hawalifurahii.”
Kuficha au kutokuficha, wataalamu wanasema
kwamba suala la kutoa milio/miguno wakati wa
tendo la kujamiiana sio suala la binaadamu peke
yao, utafiti kwa wanyama umebaini kwamba hata
manyani jike (baboons) hutoa milio fulani kabla
au wakati wa tendo hilo. Nyani jike hutoa milio
fulani kuhashiria kwa nyani dume kwamba yupo
tayari kwa tendo hilo na pia manyani jike
huongeza milio wakati wanajamiiana na nyani
dume, ambae ana cheo katika kundi lao (higher-
ranked male baboon). Zaidi ya hayo, nyani jike
aina ya “Macaque” amebainika pia kutoa milio/
miguno wakati wa tendo hili nyeti, ili kumfikisha
mwenza wake kileleni haraka!
Mwisho wa yote wataalamu wanamalizia kusema
kwamba suala la kuridhishana kimapenzi (tuite
“ukijogoo” wa mwanaume au vinginevyo), ni suala
muhimu kwa pande zote mbili, yaaani mwanaume
na mwanamke. Kwahiyo basi, suala la kutoa milio
sio tu suala la mwanamke kudanganya au
kufanya mambo asiyotaka, bali ni suala la kuwepo
“hai” (sexually present) (mara ngani umeshasikia
wanaume wa kitanzania wakilalamika kuhusu
wanawake wanaokaa kama “gogo” au “kusoma
gazeti” wakati wa kujamiiana??) wakati wa tendo
hilo na kubadilishana mahaba na mwenza wake.
Mwisho kabisa, wanasema, “wote (wanaume na
wanawake) tutoe milio!”
Je unakubaliana na utafiti huu?
Source: CNN Health
Muandaaji: www.thehabari.com

No comments:

Post a Comment